Joy FM

Shughuri za uvuvi zasitishwa ziwa Tanganyika

9 January 2024, 18:06

Waziri  wa  Mifugo  na Uvuvi  Mh. Abdalah Ulega ametangaza rasmi kusitishwa kwa shughuli za uvuvi ndani ya Ziwa Tanganyika  ili kulinda mazalia ya Samaki ambayo yanazidi kupotea huku akiwatoa hofu wavuvi kuhusu shughuli gani watakazofanya pale utekelezaji huu utakapoanza.

Na, Josephine Kiravu
Ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akitamka rasmi kusitishwa kwa shughuli za uvuvi Ziwa Tanganyika.
Awali akizungumza na kamati ya Uvuvi Mkoa wa Kigoma pamoja na viongozi kutoka Wizara hiyo amesema bila ya kusitisha shughuli za uvuvi ndani ya Ziwa Tanganyika huenda mazalia yaliyopo hivi Sasa yakatoweka kabisa.

Waziri Ulega

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti amesema wananchi hawana budi kupokea usitishwaji  huo  ili  kulinda rasilimali zilizopo kwa ajili ya kizazi kijacho.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Paul Deogratius pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Ambakisye Sintoe  wamesema Hali ya Uvuvi imeshuka kwa zaidi ya asilimia 42 huku chanzo kikitajwa kuwa ni uvuvi haramu pamoja na matumizi ya nyavu zisizo halali.

Nao  baadhi  ya wabunge akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Kirumbe N’genda wamewataka wananchi kupokea usitishwaji wa shughuli za uvuvi kwani kwa sasa samaki wanaovuliwa  ni  wadogo na kuwa hali hiyo ikiendelea huenda mazalia ya Samaki yakawa hafifu na Ziwa Tanganyika kusalia tu kwa ajili ya usafiri.

Hata hivyo baadhi ya wavuvi wameonyesha kutokubaliana na agizo la Waziri wa Mifugo na  uvuvi.

wavuvi

Mwaka jana mwezi may Serikali ilitangaza kusitishwa kwa shughuli za uvuvi ndani ya Ziwa Tanganyika kwa kipindi Cha miezi 3, licha ya  utekelezaji  huo kutofanyika kutokana na mvutano uliokuwepo baina ya baadhi ya wabunge lakini pia wananchi wakihitaji kupatiwa shughuli mbadala pale shughuli za uvuvi zitakapositishwa.

Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na katibu tawala Wilaya Kigoma wametakiwa kufuatilia watumishi watatu ambao wanawatoza pesa wavuvi na wafanyabiashara wa dagaa na samaki bila kutoa lisiti.

Sauti ya Naibu Waziri Alexander Mnyeti

.