RC Kigoma aagiza shule zote kutoa chakula kwa wanafunzi
8 January 2024, 17:31
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, amefanya ziara ya Kushitukiza kwa Baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Halmashauri za Wilaya ya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji, na kuagiza shule zote kuweka Mipango ya kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi kwa lengo la kuwawezesha kusoma kwa bidii na kukuza taaluma.
Na Tryphone Odace
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Andengenye amesema hayo wakati akikaguza hali ya wanafunzi kuanza msimu wa masomo katika mwaka wa 2024, ambapo amesisitiza suala la chakula kutolewa katika shule zote za msingi na Sekondari na kwamba Wazazi na Walimu wahakikishe suala hilo linafanikiwa.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Andengenye, amewataka walimu kuwa na Tabia Njema, itakayo kuwa mfano kwa wanafunzi kwa kuwa na wanafunzi wenye weredi katika maisha ya shule na kuwa na heshimia katika kijamii.
Hata hivyo Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya Kujifunzia Kwa wanafunzi ikiwemo kujenga miundombinu bora na kuongeza walimu licha ya baadhi ya shule kukosa walimu hasa wa masomo yamasomo ya Sayansi ambapo baadhi ya walimu na wazazi wameeleza kusapoti elimu kwa ukamilifu ikiwemo utoaji wa chakula shuleni.
.