Joy FM

Kaya zaidi ya 300 hazina mahali pa kuishi Uvinza

4 January 2024, 13:51

Wananchi kutoka katika kaya zaidi ya 300 katika kitongoji cha Kazaroho Kijiji cha Chakuru wilaya ya Uvinza hazina mahali pa kuishi baada ya serikali kuwaondoa katika maeneo waliyokuwa wakiishi tangu mwaka 2021 ambayo ni sehemu ya ya ranchi ya Uvinza.

Wananchi  hao  ambao ni wakulima  na  wafugaji wameishutumu  Serikali  kwa hatua ya kuwaondoa katika makazi yao ambayo wamedai kuwa walipewa maeneo hayo na serikali yenyewe kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki mnamo mwaka 2012 kwa ajili ya makazi.

Hata  hivyo wameshangaa kuona serikali kutumia nguvu kuwaondoa  na  kuwabomolea  nyumba zao na kuharibu mali zao ambapo kwa sasa familia zao zinalala kwenye mahema.

wananchi

Kutokana  na hali hiyo wananchi hao wameiomba Serikali kupitia  kwa  Rais Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati suala hilo ili warudishwe katika makazi yao kwa kuwa kila siku maisha yao yanazidi kuwa magumu.

Wananchi

Akitoa  taarifa kwenye kikao cha baraza la wazee wa CCM mkoa Kigoma Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, amesema kwa sasa eneo hilo liko chini ya Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO kwa usimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza.

Mkuu wa mkoa :Kamishina Jenerali wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye