Wazazi, walezi watakiwa kuimarisha ulinzi kwa watoto kipindi cha sikukuu
22 December 2023, 17:03
Na Orida Sayon
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi mkoani Kigoma kuimarisha ulinzi na usalama kwa watoto katika kipindi hiki cha sikukuu za Kristmas na Mwaka Mpya ili kuwalinda dhidi ya vitendo vinavyowaweka katika mazingira hatarishi.
Wito huo umetolewa na Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Kigoma ujiji, Mkoani Kigoma Bw. Kelvin Kusaya wakati akizungumza na redio joy fm ambapo amesisitiza kuwa katika kipindi cha sikukuu watoto wanapaswa kulindwa ili kuepusha na vitendo vya ukatili.
Bwana Kelvin ameongeza kuwa mkoa wa Kigoma kwa muda mrefu umekuwa na wimbi kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na serikali kupitiwa ofisi za ustawi wa jamii imeweza kuwarudisha watoto hao kwao na bado mchakato huo unaendelea.
Baadhi ya wazazi wakiongea na Joy fm wameeleza namna gani wanahakikisha usalama wa watoto na kushauri wazazi kulinda watoto katika msimu huu wa sikukuu.
Aidha wameongeza kuwa viongozi wa nyumba za ibada hawana budi kuweka mikakati na miundombinu itakayowawezesha watoto kusherehekea sikuu wakiwa maeneo ya ibada kwenye mikesha ili kutunza maadili kwa watoto.