Chama cha ushirika Kasulu chawachagua viongozi wapya
18 December 2023, 15:46
Chama cha Ushirika cha Umoja ni imani wilayani Kasulu mkoani Kigoma kimechagua uongozi mpya utakaodumu kwa miaka mitatu ukiongozwa na mwenyekiti wake Alfa Obed aliyechaguliwa kwa kura 106.
Na, Hagai Luyagila
Akizungumza na vyombo vya habari Afisa ushirika wa halmashauri ya Mji Kasulu Ibrahimu Katenza wakati wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho amesema halmashauri ya Mji kasulu iko tayari kutoa ushirikiano kwa chama hicho.
Aidha Katenza amesema wajumbe wa bodi hiyo waliochaguliwa mwenyekititi ni Alfa Obedi, Kaimu mwenyekiti ni Daudi Lusomi Katibu wa muda ni Stanford Lulahiye huku wajumbe wengine wa bodi ni Easther Gwambiye na Evelina Chiza sambamba na kuwataka kusimamia majukumu yao mapya
Kwa upande wake Halima Abubakari Afisa kilimo halmashauri ya Mji Kasulu amewataka viongozi waliochaguliwa kutimiza wajibu wao ili kufanikisha mikakati iliyowekwa na chama hicho katika uongozi wao.
Pia mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Umoja ni Imani Alfa Obedi amewashukuru wanachama na kuwaomba kuwa kitu kimoja pasipo kubaguana ili kuendelea kuwa kitu kimoja na kutimiza malengo waliyojiwekea.
Nao baadhi ya wanachama wa chama cha ushirika umoja ni imani Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wamesema wanaimani na viongozi waliowachaguliwa.