Ahukumiwa miaka 105 kwa makosa ya ulawiti na ubakaji uvinza
11 December 2023, 17:08
Wahukumiwa kwa makosa ya ulawiti na ubakaji Kigoma.
Na Josephine Kiravu.
Katika kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, Mahakama ya wilaya Uvinza imemhukumu kifungo cha kwenda jela miaka 105 Wangala Maganga baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kubaka na kulawiti.
Akizungumza na wanahabari wakati akieleza mafanikio ya jeshi hilo kwa kipindi cha kuanzia Novemba 20 hadi Disemba 10 Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma ACP Filemon Makungu amesema mshtakiwa huyo amehukumiwa kifungo cha miaka 105 katika vifungo vitatu tofauti.
Aidha Mahakama ya Wilaya Kasulu imemhukumu kifungo cha kwenda jela kwa miaka 30 Mshtakiwa Jackson Elias Miaka 36 Mkazi wa Kumnyika baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa jamhuri na kumtia hatiani kwa kosa la kujaribu kubaka mtoto wa kike mwenye miaka 13.
Katika hatua nyingine, Jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa watatu wanaojihusisha na matukioa ya wizi wa pikipiki.
Jeshi la polisi limeendelea kuwasihi wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kuzuia na kubaini wahalifu huku likiwataka pia wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kipindi hiki ambapo mvua zimekuwa zikinyesha na kuleta maafa katika baadhi ya maeneo.