Wajasiriamali mkoa wa Kigoma kujulikana kimataifa
27 November 2023, 15:33
Wajasiriamali wanaofanya shughuli za uokaji bidhaa manispaa ya Kigoma Ujiji wamekutana kwa ajili ya mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Shirika la viwango Tanzania TBS yenye lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.
Na, Josephine Kiravu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa kigoma, Afisa biashara na Uwekezaji Mkoa wa Kigoma Deograthias Sangu amewataka wajasiariamali hao kutumia mafunzo watakayopata kwa ajili ya kujulikana Kimataifa zaidi.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya magharibi Hamisi Sereleko amesema wanaamini kupitia mafunzo hayo wajasiariamali wataongeza ufanisi na bidhaa zao zitakuwa na ubora unaotakiwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli amesema mafunzo yamekuja muda muafaka kwani mkoa umeanza kujitanua kiuchumi na tayari wawekezaji kadhaa wameanza kuwekeza mkoani hapa.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Jenoviva Mtiti kutoka Chemba ya biashara na Kilimo pamoja na Shiza Athumani ambaye ni meneja wa Mazana wameshukuru ujio na wamafunzo hayo na kwanza utasaidia kuwaunganisha na soko la Afrika Mashariki.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanawalenga wajasiriamali wanaooka bidhaa kama vile mikate, keki, maandazi, skonzi na vingine vingi huku wachakataji wa maziwa nao wakiandaliwa mafunzo yao maalum yatakayowasaidia kwenye utendaji kazi wao.