Takukuru yabaini mapungufu kwenye miradi minne ya maendeleo Kigoma
8 November 2023, 13:39
Vitendo vya rushwa vimeendelea kushamiri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchi hali inayochangia baadhi ya miradi hiyo kushindwa kukamilika kwa wakati.
Na, Lucas Hoha
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Kigoma imebaini mapungufu kwenye miradi 4 ya maendeleo yenye zaidi ya shilingi bilioni 3 kati ya miradi ya maendeleo 33 yenye zaidi ya shilingi bilioni 12 iliyofuatiliwa na taasisi hiyo katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Septemba 2023.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa dawati la Elimu kwa Umma Takukuru Mkoa wa Kigoma, Bi. Leonida Mshema amesema mapungufu hayo ni pamoja na baadhi ya watumishi wasio waaminifu kununua vifaa vya ujenzi ambavyo havina ubora katika miradi mbalimbli ikiwemo miradi ya Boost.
Katika hatua nyingine Takukuru Mkoa wa Kigoma imeibua kero 117 kutoka kwenye kata 15 za Mkoa wa Kigoma ambapo kero hizo zisipotatuliwa kwa wakati zinaweza kusababisha vitendo vya rushwa na kuwa kero hizo wananchi wanalalamikia miundombinu ya ikiwemo ya Maji, Afya,na Elimu.
Hata hivyo wito umetolewa kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma kubadili mtazamo na kutoliona jukumu la kupambana na rushwa kama jukumu la takukuru peke yake bali wajue ni wajibu na hivyo kuwa na utayari wa kuunga mkono juhudi za mapambano dhidi ya rushwa.