Wakristo watakiwa kutumia maandiko ya biblia kukemea ukatili kwenye jamii
6 November 2023, 14:33
Katika kukabiliana na vitendo vya ukatili kwenye jamii wanachama wa chama cha Biblia tawi la kigoma wamesema chama hicho kimekuwa saada kwa kutoa elimu kwa jamii ili kuwa na hofu ya mungu.
Na, Lucas Hoha
Wakiristo mkoani Kigoma wameshauriwa kuzingatia maandiko ya biblia ili kuwasaidia kupambana na matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakisumbua jamii ikiwemo ukatili wa kijinsia ili waweze kuishi katika maadili mema.
Kila ifikapo November 5 kila Mwaka chama hicho kote duniani wamekuwa wakifanya maadhimisho ya chama yenye lengo la kutathimi kwa namna gani wamefikia malengo yao katika kuisaidia jamii na hapa wanachama wa chama hicho Mkoa wa Kigoma wanatoa wito kwa wananchi wa mkoa huo.
Mgeni rasmi kwenye Maadhimisho hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Joy in the Harvest na Radio Joy Ndugu Mwenge Muyombi amesema shirika hilo liko tayari kushirikiana na chama hicho kufikisha huduma kwa jamii hasa wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Awali akisoma lisala kwa Mgeni rasmi, Katibu wa chama hicho Manispaa ya Kigoma Ujiji, Salame Gilbert anasema chama hicho kinafanya kazi ya kuhudumia jamii ikiwemo kuwasaidia waliotelekezwa na familia zao.
Masuala mengine ambayo yamejadiliwa katika maadhimisho hayo ni wananchama kuwa na moyo wa kujitolea kuchangia fedha, ili zitumike kulitangaza neno la Mungu na waweze kujenga ofisi ili isaidie jamii waliopo kwenye mazingira rafiki.