Kiwanda cha kutengeneza meli kujengwa Kigoma
11 October 2023, 17:13
Hatua ya kuanza ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza meli kinatjwa kuwa ni miongoni mwa mikakati ya Serikali kuboresha huduma za usafirishaji ndani ya Ziwa Tanganyika.
Na, Tryphone Odace
Serikali Kupitia Wizara ya Uchukuzi, imetia Saini makubaliano ya kuanza ujenzi wa Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza Meli Nchini Pamoja na Meli mbili za Mizigo katika ziwa Tanganyika na Victoria miradi ambayo imegharimu zaidi ya Bilioni 600.
Ujenzi wa Miradi hiyo unatazamwa kuwa hatua Muhumu ya kuinua uchumi wa Mkoa wa Kigoma na Taifa kupitia mzunguko wa biashara kwa nchi za Maziwa Makuu.
Katika Hafla ya utiaji saini wa mikata mitatu ya Ujenzi wa Kiwanda cha Kujengea Meli na Ujenzi wa Meli Mbili, Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa ameagiza miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Thobias Andengenye amesema hatua hiyo ni dalili ya kufungua mkoa wa kigoma na kuwa kitovu cha biashara, wakati Mwakilishi wa Mkurugenzi Shirika la uwakala wa Meli Nchini TASAC Nelson Mlali akieleza kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa meli hizo kwa ufanisi.