Wanafunzi walio nje ya mfumo rasmi wa elimu walia na uhaba wa mabweni
11 October 2023, 12:14
Wanafunzi wanaosomo masomu ya elimu ya watu wazima wakiwemo waliorudi shule baada ya kushindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito wamesema licha ya Srikali kuwarudisha shuleni kusoma bado wanakabiliwa na mazingira magumu kutokana na wengi wao kuishi mbali na hivyo kuomba Serikali kuwajengea mabweni.
Na, Tryphone Odace
Wanafunzi waliopo katika mfumo wa elimu ya watu wazima wanaosoma katika shue ya Sekondari Mwananchi Manispaa ya Kigoma ujiji wameiomba Serikali kuweka mazingira rafiki hasa mabweni ya kulala ili waweze kuondokana na chamgamoto ambazo zilisababisha kusitisha masomo hapo awali.
Wakizungumza na Kituo hiki wakati mara baada ya shehere za maadhimisho ya siku ya elimu ya watu wazima, wamesema kuwa licha Serikali kuwapa nafasi ya kurudi shuleni kusoma wengi wao wamekuwa wakishindwa kuendeea vizuri kutokana na changamoto za maisha magumu.
“tunafurahi kuona serikali imetupa nafasi ya kurudi shule kusoma laikini wengi wetu tnakabiliwa na changamoto mbalimbali za kutoka mbali na hivyo kujikuta tunaishi katika mazingira ambayo bado yana vikwazo kama tulivyopitia kipindi tunaacha masomo, maisha magumu lakini kama watatujengea bweni tutaendelea kufanya vizuri zaidi”
Naye mratibu wa Kituo hicho ambaye pia ni mwalimu wa shule ya Sekondari Mwananchi Bw. Deogratias Ammy amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo ni vema serikali kuweka mpango wa mabweni kwa wanafunzi ambao wapo nje ya mfumo rasmi wa elimu.
wengi wanafanya vizuri sana lakini naona bado wanakuja shule wakifikiria namna ya kurudi kutokana na umbali na nadhani hii inaweza kuendelea kumwathiri kwa kuwa anapita mazingira yaleyale ambayo yana vishawishi vingi”
Kwa upande wakeMkufunzi Mkazi kutoka Taasisi ya Elimu ya watu wazima Samson Mabula amesema baada Serikali kuweka mfumo wa watoto wa kike waliojifungua wakiwa shule umewasaida wengi kujitambua licha ya changamoto za mazingira wanaoishi.
Haya yote yanajiri wakati wa maadhimisho ya elimu ya watu wazima ambapo kwa Manispa yamefanyika katia kituo cha shule ya Sekondari Mwananchi ikiwa ni miongoni mwa vituo vinavyota elimu ya watu wazima wakiwemo watoto wa kike walioacha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito.