Wafanyabiashara watakiwa kutoa stakabadhi za EFDs Kigoma
13 September 2023, 13:07
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara kuendelea kutoa stakabadhi za EFD kwa mujibu wa sheria ili serikali iweze kupata mapato kwa maendeleo ya nchi.
Na, Lucas Hoha.
Wafanyabiashara mkoani Kigoma wameaswa kutoa stakabadhi (risiti) za mashine ya kielektroniki EFD kwa wanunuzi wa bidhaa zao ili kuisaidia serikali kukusanya mapato na kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Kigoma Deogratius Shuma wakati akizungumza na kituo hiki na kuwa wafanyabiashara na wananchi wakiwa na utamaduni wa kutoa na kudai risiti serikali itakusanya mapato ya kutosha.
Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa kodi TRA Mkoa wa Kigoma Makilo Lukurunge amesema kuna kila sababu za wafanyabiashara kutoa listi amabazo ni halali na kwa wakati ili kuepusha udanganyifu wa kutoa kodi ya serikali.
Nao baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamekuwa na maoni tofauti kuhusu suala la kudai lisiti baada ya kununua bidhaa huku baadhi wakisema wanadai lisisti na wengine hawadai lisiti kwani hawajui umuhimu wake.