TPA Kigoma yadhamiria kuboresha usafirishji mafuta kwenda Burundi
1 September 2023, 11:41
Katika kuboresha huduma za usafirishaji, Mamlaka ya Bandari Tanzania mkoani Kigoma imesema inaendelea kuboresha usafirishaji wa mafuta kwa nchi ya Burundi.
Na, Tryphone Odace
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA mkoa wa Kigoma, imeanza kuchukua hatua za kuboresha nyanja za usafirishaji wa mafuta kwa nchi ya Burundi, ili kuongeza uhusiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Burundi.
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Edwadi Mabula amesema kutokana na uhitaji wa mafuta kwa nchi ya Burundi, Tanzania inatumia nafasi hiyo kufungua Slsoko la mafuta na kuongeza uhusiano wa biashra na kukuza uchumi.
Akizungumzia maboresho ya matenki ya kuhifadhi mafuta yaliyopo eneo la Kibirizi, Mabula amesema hatua zinaendelea kwa kushirikiana na mashirika ya kusambaza mafuta, kwa kuboresha miundombinu hiyo ili kuanza biashara ya mafuta mara moja.