Vyombo visivyokidhi vigezo kuondolewa ziwa Tanganyika
24 August 2023, 15:37
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoa wa Kigoma, Limezindua kampeni ya Operasheni Maboya katika ziwa Tanganyika, ili kubaini Boti zisizo na Vifaa vya Kusafiria Kwa Wavuvi na Abiria ili kuwachukulia hatua za kisheria.
Na, Kadislaus Ezekiel
Afisa mfawidhi shirika hilo mkoa wa Kigoma Abedi Mwanga amesema, wataviondoa vyombo vyote visivyokidhi vigezo vya kufanya shughuli za usafirishaji katika ziwa Tanganyika.
Aidha ameongeza kuwa tayari elimu imetolewa kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na wavuvi, hivyo hategemei kuona miongoni mwao wanavunja sheria ili kuhakikisha usalama kwa wasafiri na wasafirishaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wavuvi Mwalo wa Katonga Athuman Juma, amesema kitendo hicho kinaongeza usalama kwa wavuvi, pamoja na kuomba elimu izidi kutolewa ili kutambua umuhimu wa kutumia boya.