Wakimbizi Nyarugusu wagoma kurudi kwao, waitaka nchi ya tatu
3 August 2023, 10:17
Wakati serikali ya Tanzania na Burundi kwa kushirikiana na maashirika ya kuhudumia wakimbizi wakiendelea kuhamasisha wakimbizi kutoka Burundi ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu kurudi kwao, wakimbizi hao wamesema wanaogopa kurudi kwao kutokana na ukosefu wa mashamba ya kuishi.
Na, Tryphone Odace
Wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamesema wapo tayari kurejea nchini Burundi ikiwa matataizo ya kivita yaliyotokana na siasa na migogoro ya kifamilia itashughulikiwa na serikali ya Burundi, na kwamba hatua hiyo itawafanya waweze kurudi kwa wingi nchini mwao na kuungana na ndugu zao kujenga taifa la Burundi.
Wamesema hayo wakati wa ziara ya katibu mkuu Eizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ya Burundi, pamoja na viongozi wengine alipotembelea kambi ya Nyarugusu na ujumbe wa kuhamasiaha ndugu zao kurejea nchini Burundi.
Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Burundi Calinie Ndabarushimana amewatoa hofu wakimbizi kuwa Burundi Iko shwari.
Aidha mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Izack Mwakisu amesema wakimbizi hawanabudi kurudi kwao wakati mkurugenzi idara ya Wakimbizi Wizara ya mambo ya ndani Sudi Mwakibasi akieleza kuwa wakimbizi wanaendelea kujiandikisha na waweze kurejea nchi mwao.