Waendesha pikipiki walia na mikataba kandamizi Kigoma
19 July 2023, 11:17
Shughuli ya uendeshaji wa pikipiki maarufu bodaboda kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa na mchango mkubwa kwa vijana kujipatia kipato kwa kusafirisha abiria huku wengi wao wakipewa pikipiki hizo kwa mikataba hali iayosababisha kutofikia malengo yao.
Na,Hagai Ruyagila
Vijana waendesha piki piki maarufu boda boda Kata ya Mwandiga Halmashauri ya wilaya ya Kigoma wamemwomba mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Assa Makanika kuona namna ya kuwasaidia kupata leseni pamoja na piki piki za mikopo ili kuondokana na changamoto za mikataba inayo wakandamiza.
Wametoa maombi hayo baada ya kuzungumza na redio Joy FM ambapo wameomba mbunge huyo kuona namna atakavyowasaidia kutatua changamoto hizo kwani zimewatesa kwa miaka mingi.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe, Assa Makanika amesema yuko tayari kuwasaidia vijana hao na tayari ameshaongea na Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ili kuwasaidia kuondokana na adha hiyo.
Sambamba na hilo Mhe. Makanika amezungumzia namna ya kuwasaidia kuondokana na mikataba kandamizi kwa madereva pikipiki maarufu boda boda.
Vijana waendesha pikipiki maarufu boda boda wamekuwa na umuhimu mkubwa katika jamii tangu shughuli ya undeshaji boda boda ilipoanza na kuwa sehemu ya ajira kwa vijana walio wengi.