Watu 29 mbaroni kwa tuhuma za ramli chonganishi Mkoani Kigoma
18 July 2023, 16:16
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limesema litaendelea kutoa elimu kwa jamii kuachana na vitendo vya ramli chonganishi ambavyo husababisha uvunjfu wa amani.
Na, Josephine Kiravu
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watuhumiwa 29 wakiwa na vifaa vya kufanyia ramli chonganishi katika maeneo ya Kalalangabo kata ya Kibirizi pamoja na maeneo jirani ya mwambao mwa ziwa Tanganyika.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Philemon Makungu amethibitisha kukamatwa kwa wapiga ramli hao ambao wanatajwa kuwa chanzo cha migogoro na uhalifu ndani ya jamii ikiwemo mauaji na ukatili wa kijinsia.
Kamanda Makungu amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wasiendelee kuwapokea wapiga ramli chonganishi kwani watu hao wapo kwa ajili ya kujipatia fedha na si vinginevyo.
Na hizi zinatajwa kuwa huenda ni chanzo cha wananchi kuhitaji huduma ya ramli chonganishi kutoka kwa waganga hao kama anavyoeleza mkazi huyu wa Katombo Kata ya Mgaraganza.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limeendelea kukemea vitendo hivyo vya ramli chonganishi Mkoani Kigoma na kwamba atakaebainika kujihusisha ama kuwakaribisha waganga hao hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kuwafikisha mahakamani.