Wananchi wametakiwa kununua vipodozi kwenye maduka yaliyoruhusiwa
18 July 2023, 11:23
Shirika la viwango Tanzania TBS limesema litaendelea kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaouza bidha zilizopigwa marufuku ili kuepusha matumizi ya vipodozi visivyokidhi viwango kutumika kwa wananchi.
Na, Lucas Hoha
Wananchi Mkoani Kigoma wametakiwa kununua vipodozi kwenye maduka ambayo yameruhusiwa na wahakikishe kama vipodozi hivyo vina nembo ya TBS, ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtumiaji ikiwemo kupata Kansa ya ngozi.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Shirika la Viwango Tanzania TBS Mkoa wa Kigoma Rodney Alananga wakati akizungumza na kituo hiki akiwa Ofisini kwake ambapo amewaasa wananchi kuuliza na kupata taarifa sahihi za kipodozi kabla ya kuvitumia, huku akitaja baadhi ya vipotozi ambavyo vimepigwa mafuruku.
Aidha Alananga amekemea tabia ya baadhi ya watu ambao sio waaminifu wanaoingiza nchini vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku na serikali kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria huku akianisha baadhi ya adhabu ambazo mtu atakumbana nazo pindi akikamatwa .
Kwa upande wao baadhi wananchi wa Mkoa wa Kigoma ambao ni watumiaji wa vipodozi wamekiri kutokuwa na uelewa wa kutambua vipodozi ambavyo nisahihi kwa matumizi na ambavyo siyo sahihi.