Vijana wa JKT Bulombora wametakiwa kuwa wazalendo kwa Taifa
11 July 2023, 13:39
Vijana wa Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa JKT Bulombora kilichopo Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kuwa wazalendo kwa kulitumikia Taifa na kulinda amani ya Nchi.
Na, Kadislaus Ezekiel
Jeshi la Kujenga Taifa JKT, kikosi cha Jeshi 821 KJ Bulombora Kimesema kitaendelea Kuzalisha Vijana wenye nidhamu ya kulitumikia Taifa, uzalendo wa kutunza amani na kushiriki katika uzalishaji mali.
Naibu Kamanda kikosi cha Jeshi 24 Meja Heri Mbuma amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa, JKT ambapo ameeleza kuwa JKT ni chombo imara cha kusaidia vijana wa kulitumikia Taifa.
Kaimu Kamanda kikosi 821 KJ Bulombora Luteni Rashidi Kiliza amesema katika kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa JKT kikosi hicho kimeshiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo usafi na kupanda miti maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma.
Baadhi ya Vijana wanaopata mafunzo ya Kijeshi katika kambi hiyo wamepongeza hatua zinazochukuliwa na JKT Kwa kuwajengea uwezo wa kutambua majukumu ya kulitumikia Taifa na kujiepusha na makundi ya uvunjifu wa amani.