Wazazi, walezi watakiwa kuwalinda watoto dhidi ya ukatili
6 January 2025, 16:05
Katika kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa watoto, jamii imetakiwa kuendelea kuwalinda na kuwakinga watoto na mazingira yanayoweza kuwaingiza kwenye kufanyiwa vitendo hivyo.
Na Hagai Ruyagila -Kasulu
Wazazi na walezi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kuwakinga na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii inayowazunguka.
Jukumu la kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni wajibu wa kila mwanajamii kushiriki katika utoaji wa taarifa wa vitendo hivyo kwa ajili ya ustawi bora na maendeleo ya taifa.
Katika kilele cha wiki ya watoto Chipukizi wa injili (CWI) wa kanisa la EAGT BEROYA Mjini Kasulu Katibu wa mtandao wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia SMAUJATA Mkoa wa Kigoma Steven Kwiyanga ametumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wazazi na watoto wao kuhakikisha wanaripoti vitendo vya ukatili vinavyotokea katika jamii.
Kwa upande wake Mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT BEROYA Geofrey Kabalibali amesema elimu hiyo itasiaidia jamii kujua namna ya kubabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Naye mlezi wa idara ya watoto katika kanisa hilo ameelezea njia bora wanayoitumia ili kuwakinga watoto wao na vitendo vya vya ukatili.
Nao baadhi ya watoto Chipukizi wa injili (CWI) wa kanisa la EAGT BEROYA wamesema wako tayari kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia pindi watakapoona vitendo hivyo vikifanyika ili kupunguza changamoto hiyo.