Joy FM

Wananchi watakiwa kutumia maji safi kuepuka kipindupindu Kigoma

6 November 2024, 09:35

Wananchi wakiendelea kuchota maji katika chanzo cha maji Rutale Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Mtandao

Wananchi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, wametakiwa kutumia maji safi na salama kwa matumizi ya kunywa kutoka kwenye  vyanzo sahihi vya maji ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu.

Hayo yamesemwa na afisa afya Mkoa wa Kigoma Bw. Nesphori Fikiri Sungu wakati akizungumza na Radio Joy Fm ambapo ameeleza kuwa kumekuwepo na mlipuko wa kipindupindu sababu zikitajwa kuwa ni wananchi kutumia  vyanzo vya maji visivyokuwa safi na salama.

Sauti ya afisa afya mkoa wa Kigoma Bw Nesphori fikiri Sungu

Bw. Sungu amesema viongozi wote wa kaya mkoani kigoma hawana budi kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora kama sehemu ya  kuendelea kulinda afya za watu wengine.

Sauti ya afisa afya mkoa wa Kigoma Bw Nesphori fikiri Sungu

Hata hivyo amesema kuwa halmashauri ya wilaya kigoma imekuwa ikitoa visa vingi vya ungonjwa kipindupindu huku ikiwa kata ya kitongoni na kata ya majengo zimetoa wagonjwa wawili.

Sauti ya afisa afya mkoa wa Kigoma Bw Nesphori fikiri Sungu