Joy FM

Wahudumu wa afya watakiwa kutoa elimu ya uzazi Kasulu

5 November 2024, 13:09

Muonekano wa jengo la utawala la halmashauri ya Mji wa Kasulu Mmkaoni Kigoma. Picha na Mtandao

Serikali kupitia idara ya katika Halmashauri ya mji wa Kasulu Mkoani Kigoma imewataka wanawake hasa wajawazito kuhidhuria kliniki na kutumia dawa wanazoelekezwa na wataalamu wa afya waweze kujifungu watoto wakiwa hawana matatizo.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Baadhi ya wanawake katika halmashauri ya mji Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kupitia kwa wahudumu wa afya kuendelea kutoa Elimu ya uzazi ili kupunguza matatizo wakati wa kujifungua pamoja na kuimarisha afya bora kwa mtoto anayezaliwa.

Wamesema hayo wakati wakizungumza na Radio joy kuhusu baadhi ya watoto wanaochelewa kulia baada ya kuzaliwa na kwamba hali hiyo imekuwa ikisababisha sintofahamu kwa mzazi.

Wamesema kuwa wataalamu wa afya wanatakiwa kutoa elimu kwa wanawake wajawazito kuhusu aina ya vyakula wanavyotakiwa kutumia wakati wa ujauzito ili kuongeza uwezekano wa kujifungua mtoto mwenye afya Bora.

Sauti ya baadhi ya wanawake katika halmashauri ya mji Kasulu Mkoani Kigoma

Akizungumza kwa Njia ya Simu Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Dkt. Robert Ruebangila amesema baadhi ya matatizo wakati wa kujifungua hutokana na wanawake wajawazito kushindwa kuzingatia ushauri unaotelewa na wahudumu wa afya ambapo ameitaka jamii kuzingatia lishe bora, pamoja na wanawake wajawazito kuzingatia matumizi ya dawa za Folic Acid zinazotolewa kipindi cha ujauzito wao.

Sauti ya Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Dkt. Robert Ruebangila