Joy FM

Wafungwa kufikiwa maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura

30 May 2024, 12:13

Mkurugenzi wa tume huru ya Taifa ya uchaguzi Bw Ramadhan Kailima, Picha na Lucas Hoha

Tume huru ya taifa ya uchaguzi imesema kuwa katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura wafungwa watapata nafasi ya kujiandikisha ili waweze kushiriki katika zoezi la uchaguzi mdogo mwaka huu na uchaguzi mkuu hapa mwakani.

Na Luca s Hoha -Kigoma

Zaidi  ya  wapiga  kura wapya 224,355 wanatarajia kuandikishwa  katika zoezi la uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Kigoma unaotarajiwa kufanyika mkoani kigoma tarehe 1 Julai mwaka huu kwa muda wa siku 7.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani kigoma Mkurugenzi wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi Bw Ramadhan Kailima amesema wapiga kura hao ni ongezeko la asilimia 21.50 ya wapiga kura Milioni 1,043,281 waliopo kwenye daftari la kudumu  mkoani kigoma,

Baadhi wa waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na mkurugenzi wa tume huru ya taifa ya uchaguzi, Picha Lucas Hoha

Amesema tume hiyo imechagua mkoa wa kigoma kufanyia uzinduzi huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mwamko mkubwa wa wananchi kujitokeza katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mwaka 2019/2020.

Sauti ya Mkurugenzi wa tume huru ya uchaguz

Bw. Kailima ameongeza kuwa katika zoezi hilo makundi yote yenye sifa ya kuandikishwa  yatapata haki ya kuandishwa katika daftari hilo, ikiwemo wafungwa waliohukumiwa kifungo cha chini ya miezi 6 nakuwa kwa sasa mtu anaweza kuboresha taarifa zake katika daftari hilo kwa kutumia Simu janja.

Sauti ya mkurugenzi wa tume huru ya taifa ya uchaguzi

Katika uzinduzi wa uandikishaji wa  daftari la kudumu la wapiga kura, Mgeni rasmi anatajiwa kuwa  Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa  na  baada ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura tume huru ya taifa ya uchaguzi inatarajia kuwa na wapiga kura milioni 34,746,638 kwa nchi nzima.