Serikali yapata mwarobaini ziwa Tanganyika kujaa maji
9 May 2024, 11:47
Wafanyabiashara wanaofanya biashara katika mialo mbalimbali ya ziwa tanganyika wameomba serikali kuangalia namna ya kutenga eneo rafikikwao ili waweze kufanya biashara zao kwani maeneo ya sasa yamejaa maji kutokana na ziwa kuja maji na kuvuka kingo za ziwa.
Na Lucas Hoha – Kigoma
Makamu wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Othman Masoud amewahakikishiaa wadau wa usafirishaji wa mizigo na abiria kupitia bandari za ziwa Tanganyika kuwa serikali itakabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamesababisha ziwa hilo kujaa maji na kupelekea shughuli za bandari kutofanyika kwa ufanisi.
Amesema inaendelea kuangalia namna ya kukabiliana na tatizo la maji kuja na kusababisha maeneo ya wafanyabisghara hao kuja na wafanyabiashara kulazimika kuhama.
Mhe Masoud ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati akiendelea na ziara yake mkoani kigoma kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi wa Mkoa wa kigoma na kuwa serikali inatambua mchango wa bandari katika kukuza uchumi wa nchi hivyo serikali haina budi kuboresha mazingira ya bandari ili kuwafanya wasafirishaji kujikwamua kiuchumi.
Meneja wa bandari za Ziwa Tanganyika Edward Mabula amesema athari za mvua zinazoendelea kunyesha ni kubwa katika maeneo mengi na kuwa mamlaka ya bandari kwa kushirikiana na wadau wengine wametenga fedha kwa ajili kukabiliana na mabadiliko hayo ili shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kupitia bandari za ziwa Tanganyika ziendelee kufanyika.
Awali baadhi ya wadau wa bandari ya kigoma wameomba serikali kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na changamoto ya kujaa kwa maji katika bandari hiyo ili waendelee waendelee na kufanya kazi kwani hakuna shughuli nyingine wanaitegemea zaidi ya hiyo.