Baraza la madiwani Kigoma lapitisha rasimu ya bajeti bilioni 42
22 January 2025, 11:04
Zaidi ya Bil.42 makadirio mapato na matumizi Bil 5.2 zinatokana na mapato ya ndani mwaka wa fedha 2025-2026 zikitarjiwa kuelekezwa kwenye miradi ya kimkakati
Na Luas Hoha
Baraza la madiwani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji limepitisha rasimu ya bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 42 ambayo ni makadrio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2025-2026 na shilingi bilioni 5.2 kati ya hizo zinatokana na mapato ya ndani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Kisena Mabuba akizungumza katika baraza hilo la madiwani amesema fedha hizo zitaelekezwa kwenye miradi ya kimkakati katika manispaa hiyo ikiwemo ujenzi wa ukumbi wa kisasa na kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati shuleni.
Sauti ya mkurugenzi manispaa ya Kioma Ujiji
Nao baadhi ya viongozi walioshiriki kwenye baraza hilo akiwemo katibu tawala wa Wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota na Kaimu katibu wa ccm Kigoma Mjini Emmanuel Shitobelo pamoja na mambo mengine wameshauri uongozi wa Manispaa hiyo kuwa na mpango kazi madhubuti wa kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati na kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Sauti ya Katinbu tawala wilaya ya Kigoma na katibu CCM Kigoma mjini
Baadhi ya madiwani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji akiwemo Himid Omary diwani wa kata ya kitongoni wakichangia kuhusu majeti hiyo na vipaumbele vyake wamesema kwa sasa ukusanyaji wa mapato katika manispaa hiyo umeongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita hali ambayo imepelekea manispaa kutekeleza miradi mbalimbali kupitia mapato ya ndani.
Mchanganuo wa rasimu ya bajeti ya shilingi bilioni 42 nikuwa shilingi Bilioni 5.2 zitatokana na mapato ya ndani, shilingi Bilioni 25 itakuwa ni ruzuku kutoka serikali kuu kwa ajili ya mishahara na shilingi bilioni 1.8 ni ruzuku kutoka serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo.