Joy FM

Wakuu wa kaya watakiwa kujenga vyoo bora

20 January 2025, 11:44

Muonekano wa choo kisicho bora, Picha na mtandao

Ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya inatajwa kuwa sehemu ya mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Na Michael Mpunije

Wakuu wa kaya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kujenga vyoo bora na kuzingatia kanuni za unawaji mikono ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.