Joy FM

RC Kigoma apiga marufuku ukamataji holela pikipiki

17 January 2025, 17:04

Mkuu wa Mkoa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji, Thobias Andengenye, Picha na Josephine Kiravu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amelazimika kukutana na madereva bodaboda na kusikiliza Kero zao ikiwa ni wiki moja imepita tangu waandamane na kufunga barabara wakishnikiza Jeshi la Polisi kuacha kuwakata.

Na Josephine Kiravu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji, Thobias Andengenye amepiga marufuku ukamataji holela kwa madereva wa pikipiki huku akimtaka Kamanda wa polisi mkoani hapa kuona haja ya kuwachukulia hatua za kinidhamu askari wasio waadilifu.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma wakati akizungumza na maafisa usafirishaji mkoani Kigoma ambapo licha ya kupinga vikali uakamataji holela amewataka pia madereva hao kuhakikisha wanatii sheria za usalama barabarani.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye

Awali madereva hao walitoa malalamiko yao kwa mkuu wa mkoa wakilalamikia ukamataji usiofuata utaratibu kutoka kwa jeshi la polisi pamoja na faini kubwa wanazotozwa madereva hao.

Ni madereva bodaboda waliohudhuria kikao chaMkuu wa Mkoa Kigoma, Picha na Josephine Kiravu
Sauti ya madereva hao walitoa malalamiko yao kwa mkuu wa mkoa

Hata hivyo mkuu wa mkoa amewahakikishia madereva hao kutatua changamoto zinazowakabili huku akiwataka kuendelea kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye