Madiwani walia na migogoro ya wakulima na wafugaji Kasulu
18 November 2024, 14:56
Madiwani wametakiwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili iweze kutambua mipaka ili kuwsaidia kupunguza migogoro ya ardhi katika ya wakulima na wafugaji.
Na Emmanuel Kamangu
Migogoro ya wafugaji na wakulima katika wilaya ya uinza na wilaya ya kasulu yaongezeka ikichangiwa na jamii za wafugaji na wakulima wa wilaya hizi mbili kutokujua mipaka halisi ya maeneo yao.
Akitoa taarifa juu ya maendeleo ya kata ya Rusesa Diwani wa kata hiyo Bw, Fabian Dolagi katika mkutano wa baraza la madiwani kipindi cha robo ya kwanza ya july hadi septeber 24,25 amesema kata ya rusema ambayo imepakana kwa kiasi kikubwa na wilaya ya Uvinza kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara baina ya wafugaji na wakulima jambo linalohatarisha amani ikiwemo kupoteza nguvu kazi.
Na Kufuatia taarifa hiyo ambayo imeibuliwa na Diwani wa Kata ya Rusesa ikamlazimu Mkuu wa wilaya kasulu Kanal Isack Mwakisu kuwaagiza madiwani wilayani kasulu kusimamia vizuri sheria ili kuhakikisha migogoro hiyo inaishwa.
Aidha kanali mwakisu amesema mualubaini wa kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji katika wilaya hizi mbili zinazopakana taratibu tayari za kuainisha mipaka zinaendelea ili wananchi kujua ukomo wa maeneo wanayo paswa kutumia katika shuguli za kilimo na ufugaji.
Hata hivyo kanali Mwakisu amewataka watendaji wa vijiji na kata kusimamia sheria bila woga katika kuhakikisha migogoro ya wafugaji na wakulima inapatiwa ufumbuzi