Joy FM

Walaji wa nyama hatarini kupata magonjwa bajaji kubeba nyama

4 November 2024, 14:50

Wachinjaji wa nyama wakiwa wanaendelea kuchinja katika machinjio ya wilaya Kibondo, Picha na James Jovin

Serikali kupitia bodi ya nyama kanda ya magharibi imetoa siku saba kuhakikisha wachinjaji wanyama wanafuata kanuni na taratibu katika suala la uandaji wa nyama hadi kuwafikia watumiaji ili kulinda afya za mlaji wa nyama na kuepuka magonjwa ya mlipuko vinginevyo watafungiwa kufanya shughuli hiyo.

Na James Jovin – Kibondo

Walaji wa nyama ya ng’ombe na mbuzi katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na wachinjaji katika machinjio ya wilaya hiyo kutofuata masharti na vigezo vinavyotakiwa ili kufikisha nyama buchani ikiwa safi na salama kwa mlaji.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kutumia bajaji kubebea nyama badala ya gari maalumu la nyama, wachinjaji kutopima afya, kutovaa mavazi maalumu wakati wa kuchinja na mazingira machafu yanayoonekana katika machinjio hiyo.

Baadhi ya wachinjaji wa nyama katika machinjio ya wilaya ya Kibondo wamekiri kushindwa kufuata masharti yanayotakiwa ili kuweza kuchinja nyama katika mazingira safi na salama ili kulinda afya ya mlaji wa mwisho na kuzuia magonjwa ya mlipuko.

Sauti ya baadhi ya wachinjaji wa nyama katika machinjio ya wilaya ya Kibondo

Kwa upande wake mkaguzi wa machinjio Kibondo mjini bw. Alex Lucas amekiri kuwepo kwa changamoto hizo upande wa wachinjaji lakini pia upande wa serikali ambao wanapaswa kuboresha machinjio na kuweka mazingira mazuri ili nyama iweze kutoka machinjioni na kufika buchani ikiwa safi na salama.

Sauti ya mkaguzi wa machinjio Kibondo mjini bw. Alex Lucas

Bodi ya nyama kanda ya magharibi ambayo inaendelea na ziara ya kutoa elimu kwa wachinjanji, wachunaji na wasafirishaji wa nyama katika wilaya ya Kibondo na mkoa wa Kigoma kwa ujumla kama anavyoeleza hapa Bw. Joseph Kurwa msimamizi wa bodi ya nyama kanda ya magharibi.