Joy FM

Wazazi waaswa kulea watoto katika maadili mema

9 October 2024, 11:40

Afisa elimu, elimu maalumu halmashauri ya Mji Kasulu Salvatory Kitogwe akiwa katika mahafali ya 12 ya shule ya Sekondari Rev A. Bungwa, Picha na Hagai Ruygaila

Wanafunzi wanaohitimu elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Rev. A. Bungwa iliyopo halmashauri ya mji wa kasulu wametakiwa kuwa na maadili mema kwenye jamii na kufuata misingi waliyofundishwa kwa kipindi chote walichokuwepo shuleni kwa manufaa yao ya baadaye.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Wazazi na walezi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameaswa kuwalea watoto wao katika maadili mema jambo ambalo litawasaidia kujiepusha na vitendo visivyoendana na tamaduni za kitanzania hususani ndoa ya jinsia moja.

Hayo yameelezwa na Salvatory Kitogwe afisa elimu elimu maalumu halmashauri ya Mji Kasulu wakati wa mahafari ya 12 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Rev A. Bungwa iliyopo katika halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma.

Wahitimu wa kidato Cha nne katika shule ya sekondari Rev A Bungwa, Picha na Hagai Ruyagila

Kitogwe amesema malezi bora yana umuhimu mkubwa sana kwa mtoto maana Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Sauti ya Salvatory Kitogwe afisa elimu elimu maalumu halmashauri ya Mji Kasulu

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo Bi. Perpetua Kasunzu amewasisitiza wanafunzi hao wanaoelekea kuhitimu kidato cha nne mwezi ujao kuhakikisha wanakuwa na tabia njema ambayo itawasaidia kujiepusha kutumia madawa ya kulevya.

Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Rev A Bungwa Bi. Perpetua Kasunzu, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo Bi. Perpetua Kasunzu

Naye Mkuu wa shule ya sekondari Rev A Bungwa Mwalimu Steven Kachenke amewataka wanafunzi hao kuitumia vizuri elimu waliyoipata katika maisha yao na  jamii inayowazunguka.

Mkuu wa shule ya sekondari Rev A. Bungwa Steven Kachenke, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Mkuu wa shule ya sekondari Rev A Bungwa Mwalimu Steven Kachenke

Nao wahitimu wa kidato cha nne katika shule hiyo wamesema watahakikisha wanaitumia vizuri elimu hiyo ili kuwa viongozi bora ndani ya jamii kwa kusimamia maadili mema waliyojifunza katika  shuleni hiyo.

Sauti ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Rev A. Bungwa

Shule ya sekondari Rev A. Bungwa iliyopo katika kata ya Kigondo halmashauri ya Mji Kasulu ilianzishwa mwaka 2009 na katika mahafari hayo ya 12 ya kidato cha nne jumla ya wanafunzi 97 wanatarajia kufanya mtihani wa taifa mwezi ujao.

Wazazi na walezi waliohudhuria katika mahafari hayo katika shule ya sekondari Rev A Bungwa, Picha na Hagai Ruyagila