Joy FM

Benki ya EXIM yaahidi kutoa huduma bora kwa wateja wake

4 October 2024, 17:21

Ni baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya EXIM wakikatika hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Picha na Mullovan Cheppa

Benki ya Exim tawi la Kigoma imesema itaendelea kuboresha na kutoa huduma bora kwa wateja wake huku ikiwataka wafanyabiashara na mashirika yaliyopo mkoani kigoma kujitokeza na kuomba mikopo inayotolewa na benki hiyo kwa lengo la kukuza biashara zao.

Na Joha Sultan – Kigoma

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja,  Bank ya Exim tawi la Kigoma Tanzania imewashukuru wateja wote kwa kuwa pamoja nao na kuwaahidi kuendelea kutoa huduma stahiki kwa ukaribu ili kuweza kuleta maendeleo zaidi kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa shirika la Joy In The Harvest Mwenge Muyombi akikata keki wakati wa hafla ya huduma kwa wateja iliyoandaliwa na Benki ya Exim.

Shukrani hizo zimetolewa na  Meneja wa tawi la Exim bank Kigoma ndugu Michael Tuntufye kwenye hafla fupi ambayo iliandaliwa na bank hiyo kwaajili ya kutoa shukrani kwa wateja wake.

Sauti ya Meneja wa tawi la Exim bank Kigoma ndugu Michael Tuntufye
Ni baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya EXIM wakikatika hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Picha na Mullovan Cheppa

Aidha amesema wateja ambao wanataka kupatiwa mikopo hususani mashirika pamoja na wafanyabiashara milango ya kuwakopesha iko wazi ili kuwawezesha kukuza biashara zao.

Sauti ya Meneja wa tawi la Exim bank Kigoma ndugu Michael Tuntufye

Nao baadhi ya wateja ambao ni wanufaika wa banki ya Exim wameeleza namna ambavyo banki hiyo  inavyowahudumia kwa uadilifu mkubwa bila upendeleo.

Mkurugenzi wa shirika la Joy In The Harvest Mwenge Muyombi akikata keki wakati wa hafla ya huduma kwa wateja iliyoandaliwa na Benki ya Exim.
Sauti ya baadhi ya wateja ambao ni wanufaika wa banki ya Exim tawi la kigoma