Joy FM
Joy FM
30 April 2025, 14:40

Zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga kura awamu ya pili linatarajia kuanza mei mosi.
Na Emmanuel Kamangu
Mawakala wa vyama vya siasa wametakiwa kufuata sheria na taratibu katika vituo vya uandikishaji wakati wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa uwazi na weledi.
Amebainisha hayo, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kasulu Vijijini Bw Emmanuel Ladislaus wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura halmashauri ya wilaya ya kasulu ambapo ameeleza kuwa ili kuendesha zoezi Kwa usawa mawakala wa vyama vyote vya siasa watashirikishwa kikamilifu katika zoezi huku akiwasihi washiriki wa mafunzo hayo kufuata taribu na Sheria wakati wa zoezi ikiwemo kuhakikisha wanatunza vifaa vyote vitakavyokuwa katika vituo vya uandikishaji.
Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo mmoja wao akiwa Bi Yasinta Kisunzu wamesema mafunzo Kwa kiasi kikubwa yamewajengea uwezowa kiutendaji wakati zoezi litakapoanza.
Zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili linatarajiwa kuanza Mei 1 hadi 7 mwaka huu ambapo Wananchi wote wenye sifa wataruhusiwa kujiandikisha au kuhakiki taarifa zao Kwa ajili ya kupata kitambukisho Cha mpiga kura.