Recent posts
8 February 2024, 19:59
Kigoma: Wananchi waonywa matumizi ya dawa kiholela kutibu macho mekundu
Wananchi mkoani Kigoma wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa macho mekundu, ulioripotiwa hivi karibuni kutokea katika baadhi ya mikoa mbalimbali hapa nchini. Na, Horida Sayoni Mganga mkuu wa mkoa wa kigoma Dr. Jesca Leba Amesema hayo wakati akizungumza na…
7 February 2024, 15:23
Wafanyabiashara Kasulu wahimizwa kutunza mazingira
Wafanyabiashara na wajasiriamali katika halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuwa na vitunzia taka katika maeneo yao kwa ajili ya kuhifadhi uchafu. Na, Mwandishi wetu Emmanuel Kamangu anasimulia zaidi
7 February 2024, 14:32
Halmashauri ya Kibondo kujenga jengo la ghorofa 3
Halmashauri ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imetenga shilingi bilioni 2.5 ili kujenga jengo jipya la vijana community center ikiwa ni mikakati ya kuchochea na kukuza uchumi wa halmashauri na jamii kwa ujumla Na, James Jovin Hayo yamebainishwa na diwani…
5 February 2024, 15:32
Viongozi wa dini wakemea ramli chonganishi Kigoma
Jamii imeshauriwa kutojihusisha na vitendo vya ramli chonganishi ambavyo vinafanywa na waganga wa kienyeji ili kuwatapeli wananchi. Na, Josephine Kiravu Viongozi wa dini Kutoka madhehebu mbalimbali Mkoani kigoma wamekemea vikali vitendo vinavyoendelea kufanywa na waganga wanaopiga ramli chonganishi maarufu kwa…
5 February 2024, 13:29
watoto wenye uhitaji maalum waomba kutatuliwa changamoto zao
Watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Nengo iliyoko wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhitaji wa taulo za kike hasa kwa wasichana hali ambayo wakati mwingine hupelekea kukosa masomo darasani. James Jovin ana maelezo zaidi.
2 February 2024, 09:28
Baraza la madiwani kibondo lapitisha rasmu ya bajeti ya bilioni 37.9
Halmashauri ya Wiliya Kibondo Mkoani Kigoma yapitisha rasmu ya bajeti ya mwaka 2024/2025. Na James Jovin. Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma limepitisha rasimu ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 37.9 kwa mwaka wa…
1 February 2024, 17:15
Wakandarasi wa barabara Kigoma wanyoshewa kidole kutowajibika
Wajumbe Wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Kigoma, Wamelalamikia Kusuasua kwa Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara za Uvinza – Tabora na Kigoma – Kalya, Kwa madai ya wakandarasi kutowajibika ipasavyo, Pamoja na Kiwango Duni cha Ujenzi wa Mitaro Katika Barabara…
1 February 2024, 10:49
Kigoma: Miradi ya kimkakati kuimarisha uchumi nchini, nchi jirani
Serikali imesema inaendelea kuhakikisha inaboresha miradi ya kimkakati kwenye sekta ya usafiri iliyopo ili kusaidia katika ukuaji wa uchumi hasa kupitia sekta ya usafirishaji kwa njia ya maziwa. Na, Tryphone Odace. Meneja Mipango kutoka kampuni ya huduma za meli nchini…
1 February 2024, 10:11
Nyamori kupata shule ya sekondari kwa mara ya kwanza
Wananchi wa kijiji cha Nyamori kata ya Simbo katika wilaya ya Kigoma wameipongeza serikali kwa juhudi za uboreshaji wa miundombinu ya elimu hasa ujenzi wa shule katika maeneo mbalimbali mkoani Kigoma. Wameeleza hayo wakati wakipokea mifuko 50 ya saruji kwa…
1 February 2024, 09:25
TAKUKURU yabaini mapungufu kwenye miradi 25 ya maendeleo Kigoma
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru mkoani Kigoma imebaini mapungufu kwenye miradi 25 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 9 iliyofuatiliwa katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2023. Na, Lucas Hoha Hayo yamebainishwa na…