DC Kasulu ataka ufuatiliaji usalama wa mazao ya chakula
15 January 2025, 12:34
Kutokana na umuhimu wa chakula kwa maisha ya binadamu, ustawi na maendeleo ya nchi, suala la kuhakikisha kuwa chakula ni salama kwa matumizi ya binadamu linapewa kipaumbele na kuzingatiwa kikamilifu kwa lengo la kulinda afya ya walaji na kuwezesha utoshelevu wa chakula.
Na Michael Mpunije
Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amewataka viongozi wa vijiji na kata kufuatilia usalama wa mazao ya chakula kwa wakulima ili kubaini wadudu waharibifu wanaoshambulia mazao hayo waweze kudhibitiwa.
Kanali Mwakisu Amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa na watumishi wa Serikali ya kijiji na kata Halmashauri ya wilaya ya Kasulu na kuwataka viongozi hao kufuatilia mazao ya wakulima ikiwa yanachangamoto ya kushambuliwa na wadudu waharibifu.
Amesema usalama wa chakula ni muhimu katika kuleta ustawi kwa jamii hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wataalamu wanapobaini changamoto ya mazao kushambuliwa na wadudu ili wasisababishe madhara ya ukosefu wa chakula kwa wananchi.
Aidha Kanali Mwakisu amezitaka familia kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuacha kuwa tegemezi jambo ambalo litasaidia kupunguza vitendo vya wizi na udokozi.