Wakristo watakiwa kufanya kazi kujiongezea kipato
15 January 2025, 12:09
Kufanya kazi kwa bidii na kumiliki uchumi kwa mtu mmoja mmoja kunachangia pato la nchi kuinuka na kupanda zaidi
Na Timotheo Leonard
Waumini wa Kanisa la Pentekoste Motomoto PMC tawi la Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji wameshauriwa kufanyakazi kwabidii kwalengo la kujiongezea kipato kwani kanisa linahitaji watu wachapakazi kwamanufaa ya familia,kanisa na taifa kwaujumla.
Yamebainishwa na Askofu wa Kanisa la Pentekoste Motomoto Jimbo la Tanganyika Jacksoni Maneno Gahamba wakati wa ibada ya kumuweka wakfu mchungaji Emmanuel Marko Kambi kuwa mwangalizi mpya wa kanisa hilo tawi la Kibirizi.
Askofu Gahamba amemsisitiza mwangalizi mpya kuwa miongoni mwa majukumu yake nipamoja na kuhakikisha anashirikiana na waumini kuhimiza maendeleo kwa kufanya kazi ili kujikomboa kiuchumi.
Sauti ya Askofu
Kwa upande wake Mchungaji Emmanuel Marko Kambi ambaye amewekwa wakfu kuwa mwangalizi wa kanisa hilo, ameelezea furaha aliyonayo baada ya kupata nafasi hiyo,huku akisema kila hatua anayoipiga ni kwa Msaada wa Mungu pekee.
Sauti ya mchungaji
Baadhi ya watumishi wa Mungu waliohudhuria ibada hiyo wamesema hawana budi kuungana pamoja kumpa ushirikiano mwangalizi mpya kwani ni moja ya wachapakazi mahili
Sauti za waumini