Joy FM

Miradi shikizi kukamilika kwa wakati Kigoma

14 January 2025, 12:47

Muonekano wa barabara ya Kabingo – Manyovu wakati ikitengenezwa, Picha na Mtandao

Wananchi wa Kakonko wanatarajia kupata huduma za maji, afya, shule ikiwa ni miradi shikizi katika ujenzi wa barabara kuu ya Kabingo – Manyovu.

Na Josephine Kiravu

Naibu Waziri wa ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka wakandarasi wanaosimamia miradi shikizi kupitia ujenzi wa Barabara ya manyovu-kabingo mkoani Kigoma kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati na kwa kuzingatia ubora uliokusudiwa.

Kasekenya ametoa wito huo mara baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa miradi hiyo na kusisitiza kuwa hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wakandarasi wazembe.

Naibu waziri amesema hayo mara baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya maji, afya, shule na soko katika wilaya za Buhigwe,Kasulu, Kibondo na Manyovu mkoani Kigoma

Katika ziara hii Waziri ameonesha kutoridhishwa na hali ya utekelezaji wa kazi katika baadhi ya maeneo na Kufuatia kasoro hizo Waziri akaagiza wakandarasi waliyopewa kazi hiyo kurekebisha na kuhakikisha muda uliopangwa unazingatiwa.

Sauti ya Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya

Aidha Waziri amewataka TANROADS kama wasimamizi wakuu wa miradi hii kusimamia kwa ukaribu utekelezaji ili kuepuka changamoto zilizopo kujirudia.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa barabara mkoani Kigoma Mhandisi Narcis Choma amekiri kuwepo kwa wakandarasi ambao utendaji kazi wao hauridhishi nakuahidi kushughulikia maagizo ya Naibu waziri ili miradi ikamilike kwa wakati.

Sauti ya Meneja Wakala wa barabara mkoani Kigoma Mhandisi Narcis Choma

Nao baadhi ya wananchi wanaonufaika na miradi hiyo wametoa maoni yao huku wakihimiza juhudi zaidi kufanyka ili miradi hiyo iweze kufanikisha maendeleo wanayoyatarajia.

Sauti ya baadhi ya wananchi wanaonufaika na miradi hiyo wametoa maoni yao

Miradi shikizi imegharimu takribani billion ishirini na sita ikifadhiliwa na benki ya dunia katika ujenzi wa barabara ya manyovu kabingo yenye urefu wa kilometa miambili sitini.