Viongozi wa serikali za mitaa kuhimiza wazazi kuchangia chakula shuleni
6 December 2024, 09:37
Viongozi wa serikali za mitaa wametakiwa kuhamasisha suala la chakula shuleni ili kusaidia watoto kupata chakula na kuweza kusoma vizuri.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Wenyeviti wa vijiji, vitongoji na wajumbe katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wametakiwa kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa kuhamasisha wazazi na walezi wanashiriki kikamilifu katika kampeni ya wanafunzi kupata chakula cha mchana shuleni
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu wakati akizungumza na viongozi hao katika ukumbi wa shule ya msingi Bogwe uliopo halmashauri ya mji Kasulu.
Kanal Mwakisu amesema lazima mtoto apate elimu na chakula shuleni ili kufikia ndoto zake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Kasulu Emmanuel Ladislaus amewasihi viongozi hao kuwatumikia wananchi wao kwa kutatua chagamoto zinazowakabili katika maeneo yao sambamba na kuwasomea wananchi hao mapato na matumizi.
Nao baadhi ya wenyeviti wa vijiji, vitongoji na wajumbe wa serikalu za mitaa katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu wamesema wako tayari kuhamasisha wazazi na walezi kuchagia chakula shuleni ili kuwasaidia wanafunzi kuendelea kupata chakula shuleni.