Wagombea watakiwa kufanya kampeni kwa amani Buhigwe
19 November 2024, 14:27
Kampeni za uchaguzi wa serikaili za mitaa zinazinduliwa rasmi kitaifa katika eneo la Kiganamo Hamlmashauri ya mji wa Kasulu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Wakati kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa zikienda kuzinduliwa novemba 20 kwa ajili uchaguzi wa viongozi mbali mbali wa serikali za mitaa nchini, Wananchi wilayani Buhigwe mkoani Kigoma wamewataka wagombea kufanya kampeni za kistarabu zisizokuwa na viashiria vyauvunjifu wa amani.
Wakizungumza na Radio Joy Fm, wamesema wanahitaji kampeni za viongozi wanaowania nafasi mbali mbali za uongozi wa serikali mitaa kuhakikisha kapeni zao hazileti uchanganishi kati yao bali waeleze sera za nini watakifanya iwapo watachaguliwa.
Aidha wananchi hao wamesema watamchagua kiongozi ambaye ataweza kutatua changamoto zilizopo ndani ya jamii yao huku akiisaidia serikali kusimamia miradi ya maendeleo iliyoletwa na serikali pamoja na kuibua miradi mingine ya maendeleo katika uongozi wake.
Kwa upande wake, Mchungaji kiongozi Shedrack William wa kanisa la anglikana Nyaruboza ililopo wilayani Buhigwe amesema kiongozi bora ni yule mwenye maadili mema ambaye atakubali kuwasaidia wananchi wake kupata maendeleo kuliko kupokea rushwa.
Kampeni za wagombea wa vyama vya siasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa zinatarajiwa kuzinduliwa novemba 20 mpaka 26 mwaka huu huku Uchaguzi wa serikali za mitaa ukitarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Ambapo Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu wa 2024 umebebwa na kauli mbiu isemayo serikali za mitaa sauti ya wananchi jitokezeni kushiriki uchaguzi kwa maendeleo endelevu.