Joy FM

DC Uvinza awataka wagombea waliowekewa pingamizi kukata rufaa

14 November 2024, 13:14

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Dina Mathamani, Picha na Joy Fm

Wakati muda uliowekwa kwa wagombea waliowekewa pingamizi ukikaribia kuisha, Mkuu wa Wilaya Uvinza Mkoani Kigoma ametaka wagombea kuwasilisha rufaa zao mapema kabla ya muda wa ziada kuisha.

Na Sofia Cosmas – Uvinza

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Dina Mathamani amewataka wagombea katika uchaguzi serikali za mitaa waliowekewa  pingamizi  kukata rufaa ili kupata haki zao za msingi za kugombea katika nafasi mbalimbali uchaguzi serikali za mtaa utakaofanyika novemba 27 mwaka huu.

Mh. Dina Mathamani ameeleza hayo wakati akizungumza katika kipindi cha  Goodmorning Kigoma kinachorushwa na Redio Joy Fm, ambapo amewataka wagombea uchaguzi serikali za mtaa katika wilaya ya uvinza kutumia muda ulioongezwa ili kupata haki yao ya msingi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Dina Mathamani

Aidha amewataka wananchi kuwa na uelewa ili kupata viongozi wa kijiji ambao watawatetea na kusimamia yale ambayo serikali imepanga kwa mustakabali wa taifa kwa ujumla.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Dina Mathamani

Katika hatua nyingine,  Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh. Dina Mathamani  amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Dina Mathamani

Kutokana na miundombinu ya shule kuimarishwa katika wilaya ya uvinza imepelekea ufaulu wa darasa la saba kupanda na kuibuka kididea kwa kushika nafasi ya kwanza kwa miaka miwili mfululizo.

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Dina Mathamani, Picha na Joy Fm