Joy FM

Askofu Bwatta awataka waumini kujiandikisha daftari la kura

15 October 2024, 12:12

Askofu wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwata, Picha Lucas Hoha

Viongozi wa dini wametakiwa kuendelea kuwahamasisha waumini wao kuendelea kujitokeza na kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ili waweze kupata nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.

Na Lucas Hoha – Kasulu

Askofu wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwata amewaomba waumini wa Kanisa hilo kujitokeza kujiandisha kwenye daftari la mkazi kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa ili kupata viongozi wenye hofu ya Mungu watakaokataa rushwa katika jamii  na vitendo vya ukatili kwa wananchi.

Viongozi wa kanisa la anglikani dayosisi ya western tanganyika wakiwa katika picha ya pamoja, Picha na Lucas Hoha

Hayo yamejiri katika Ibada maalumu ambayo imefanyika katika kanisa kuu la Anglikani lililopo katika Mji wa Kasulu mkoani Kigoma, iliyolenga kufungua sinodi ya 18 ya kanisa hilo na kuwawekea mikono waumini ambao wamefundishwa mafunzo ya kipaimara

Bwatta ametumia Ibada hiyo kuwakumbusha waumini kutimiza haki ya msingi ya kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ili wawe na sifa ya kupiga au kupigiwa kura kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwata

Naye Askofu wa Dayosisi ya Lake Rukwa Efraimu Ntikabuze  awali akitoa mafundisho matakatifu amesema kipindi hiki cha uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na uchaguzi wa serikali kuu mwaka 2025, kuna kila sababu ya kanisa kumuomba Mungu ili amani izidi kudumu katika Taifa la Tanzania.

Sauti ya Askofu wa Dayosisi ya Lake Rukwa Efraimu Ntikabuze

Nao baadhi wa washirika wa Kanisa hilo wamesema wamepokea hamasa ya Askofu ya kuwataka kujiandisha kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za Mitaa, nakuwa watafanya hivo ili kupata viongozi wenye hofu ya Mungu.

Sauti za baadhi wa washirika wa Kanisa hilo
Waumini wa kanisa la anglikani wakiwa katika ibaada, Picha na Lucas Hoha