Joy FM

Raia wa kigeni waonywa kutojihusisha na uchaguzi serikali za mitaa

7 October 2024, 13:33

Nembo iliyoandaliwa na ofisi ya TAMISEMI ikihamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa nchini, Picha na Mtandao

Wakati siku zikienda mbio kuelekea siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kampeni za kuhamasisha wananchi wenye siku kujitokeza na mkoa wa kigoma unatajwa kuwa miongozi mwa mikoa inayokuwa na raia wa kigeni na hivyo kutakiwa kutojihusisha kwenye uchaguzi huo.

Na James Jovin – Kibondo

Raia wa kigeni wanaoishi mpakani mwa wilaya ya Kibondo na Burundi wameonywa kutojihusisha na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba kote nchini.

Rai hiyo imetolewa na afisa uhamiaji wilaya ya Kibondo Bw. Frank Rubilo wakati wa zoezi la kuhamasisha na kutoa elimu kwa  wananchi kujiandikisha na kupiga kura zoezi linaloendelea kufanyika hasa katika vijiji vinavyopakana na nchi ya Burundi vikiwemo Kigina, Kibuye na Mukalazi.

Sauti ya afisa uhamiaji wilaya ya Kibondo Bw. Frank Rubilo

Mmoja wa wananchi mkazi wa kijiji cha Kibuye kilichoko mpakani mwa Burundi Bw. Jasson Emily  amewataka viongozi kutumia wazee wenye uzoefu katika shughuli hiyo ya uchaguzi ili kuwabaini raia wa kigeni wanaoweza kujihusisha na uchaguzi kugombea ama kuchagua wakati si raia wa Tanzania.

Sauti ya Mmoja wa wananchi mkazi wa kijiji cha Kibuye kilichoko mpakani mwa Burundi bwana Jasson Emily

Kwa upande wake Dkt. Gabriel Chitupila akimwakilisha msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Kibondo katika mkutano huo amesisitiza wananchi kuchagua viongozi watakao wavusha katika matatizo yao na hivyo kuleta maendeleo katika jamii na serikali kwa ujumla.

Sauti ya Dkt. Gabriel Chitupila akimwakilisha msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Kibondo katika mkutano huo

Halmashauri ya wilaya ya Kibondo inaendelea kutoa elimu ya uchaguzi kote wilayani humo hasa katika maeneo ya mipakani ampako kuna idadi kubwa ya raia wa kigeni huku msisitizo mkubwa ikiwa ni kuhakikisha raia hao wa kigeni hawashiriki uchaguzi huo.