Joy FM

Wadau watoa msaada wa vyakula na vifaa shule ya kasange

4 October 2024, 11:48

Ni photocopy mashine ambayo imetolewa na mdau wa maendeleo ya sekta ya elimu Kasulu Daniel Ruzino, Picha na Hagai Ruyagila

Wadau wa maendeleo wilayani kasulu mkoani kigoma wametakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kusaidia kuboresha elimu ili kusaidia watoto waweze kupata haki yao ya elimu.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma ya chakula shuleni wadau wa maendeleo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamejitolea vitu mbali mbali ikiwemo mchele, maharage na chumvi katika shule ya sekondari Kasange iliyopo kata ya Heru juu halmashauri ya Mji Kasulu ili kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa elimu bora.

Diwani wa kata ya heru juu ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Noel Hanura ni miongoni mwa wadau ambao wameshiriki zoezi hilo la utoaji wa vyakula katika shule hiyo.

Akizungumza na wazazi, wanafunzi pamoja na waalimu Bw. Hanura amesema wazazi wanatakiwa kuendelea kuchangia chakula shuleni kama serikali inavyoelekeza ambapo ametoa mchele kilo 200 kwa ajili ya waalimu, mahindi, maharage, chumvi pamoja na mafuta kwa ajili ya wanafunzi.

Sauti ya Diwani wa kata ya heru juu ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Bw. Noel Hanura

Kwa upande wake mmoja wa wadau wa maendeleo kutoka kata ya heru juu wilayani Kasulu Daniel Ruzino ametoa photocopy mashine katika shule ya sekondari Kasange kwa ajili ya kurahisisha shughuli za uchapishaji wa mitihani huku akiwasisitiza wanafunzi kuacha tabia za utoro.

Mdau wa maendeleo ya sekta ya elimu wilaya kasulu Daniel Ruzino, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya wadau wa mandeleo wilayani kasulu

Baadhi ya wanafunzi wametoa shukurani zao kwa wadau hao wa maendeleo ya sekta ya elimu kwa kuchangia chakula na photocopy mashine wamesema vitasaidia kupunguza changamoto shuleni hapo.

Sauti ya wanafunzi wametoa shukurani zao kwa wadau hao wa maendeleo ya sekta ya elimu kwa kuchangia chakula na photocopy

Nao wazazi na walezi akiwemo Jusilini Kaliye na Boniface Fyekenye wamempongeza diwani wa kata ya heru juu pamoja na mdau huyo wa maendeleo kwa kutimiza ahadi ya kuchangia chakula shuleni hapo kwani itasaidia kuongeza hasama kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii hali itakayosaidia kufanya vizuri katika masomo yao.

Sauti ya wazazi na walezi wakipongeza msaada huo