Milioni 460 zajenga nyumba 4 za watumishi wa afya Kasulu
19 September 2024, 13:39
Serikali imeesema itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa watumishi wa afya kwa kuwajengea nyumba za kuishi ili waweze kutoa huduma kwa wananchi wakiwa karibu na maeneo yao ya kazi.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Jumla ya shilingi milioni 460 zimetumika katika ujenzi wa nyumba 4 za wahudumu wa afya katika hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa mapato ya ndani.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo za watumishi wa sekta ya afya, Mhandisi wa mradi huo kutoka halmashauri ya wilaya ya Kasulu Julius Shirawi ameeleza manufaa ya mradi huo ni kuboresha na kusogeza huduma Bora za afya Kwa jamii.
Kwa upande wake, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru taifa mwaka 2024 Godfrey Mnzava ameipongeza halmashauri hiyo Kwa ujenzi Bora wa nyumba hizo za watumishi Kwa mapato ya ndani huku akiwasisitiza watumishi na kuzitunza nyumba hizo.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Dr. Semistatus Mashimba amesema ujenzi wa nyumba hizo ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha watumishi wa idara ya afya wanakata katika mazingira Bora.
Nao baadhi ya wahudumu wa afya katika halmashauri hiyo wanaotumia nyumba hizo wameipongeza serikali Kwa kuwajengea nyumba karibu kwani awali walikuwa wanakaa mbali na eneo wanapotolea huduma.
Mwenge wa uhuru mwaka 2024 umebebwa na kaulimbiu isemayo tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Kwa ujenzi wa taifa endelevu.