Joy FM

Shilingi milioni 950 zakamilisha barabara mjini Kasulu

18 September 2024, 17:06

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Eliakim Mnzava akiweka jiwa la msingi katika mradi wa barabara mjini kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024, Godfrey Eliakim Mnzava amemtaka meneja wa TARURA wilaya Ksulu kuhakikisha anaweka taa kwenye barabara ambayo imejenwa kwa gharama ya shilingi milioni 950.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Jumla ya shilingi milioni 950 kutoka serikali kuu kupitia mfuko wa Jimbo la Kasulu Mjini na tozo zimetumika kujenga mradi wa barabara kwa kiwango Cha lami GTZ  na Kiganamo  Bogwe yenye kilometa 1.1. katika halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma.

Akitoa taarifa  ya ujenzi wa barabara hiyo kiwango Cha lami meneja wa Tarura wilaya ya Kasulu Mhandisi Senzia Maenda amesema lengo la ujenzi huo ni kupunguza msongamano wa magari katika baadhi ya barabara  mjini kasulu.

Meneja wa Tarura wilaya ya Kasulu Mhandisi Senzia Maenda, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Kasulu

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Eliakim Mnzava amekagua na kuweka jiwe la msingi katika barabara hiyo ambapo ametoa maelekezo kukamilisha vitu vilivyobakia ili uweze kukamilika kama ilivyo pangwa.

Sauti ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024

Mwenge wa uhuru wa mwaka 2024 umebebwa na kaulimbiu isemayo tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Kwa ujenzi wa taifa endelevu