Joy FM

Bilioni 2.8 kujenga mradi wa maji kwa vijiji 3 Kigoma

16 September 2024, 07:20

Naibu waziri wa maji Kundo Methew akiwa na wananchi wa Kazegunga mara baada ya kutembelea mradi wa maji, Picha na blog ya KGPC

Serikali kupitia Wizara ya Maji imesema itaendelea kujenga na kupanua usambazaji wa maji kwa wananchi ili kurahisisha upatikanaji kwa jamii na kuondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji.

Na Tryphone Odace – Kigoma DC

Zaidi ya shilingi bilioni mbili zinatarajia kutumika katika ujenzi wa tenki na pampu ya maji ili kumaliza changamoto za upatikana wa maji kwa wakazi wa vijiji  vya Kazegunga, Kasaka na Msimba katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Kigoma KUWASA Poas Kilangi wakati Naibu waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew alipotembelea eneo ambalo linaratajia kujengwa mradi huo mpya wa tenki na pampu ya maji.

Naibu Waziri wa Maji Kundo Methew akikagua mashine kwenye moja ya mradi wa maji

Kilangi amesema taratibu za kumpata mkandarasi zinaendelea na mradi unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12 hatua ambayo inatajwa kuwa  itamtua mama ndoo kichwani.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Kigoma KUWASA Poas Kilangi

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew ameitaka KUWASA kuhakikisha mkandarasi anapatikana kwa wakati ndani ya mwezi mmoja ili mradi huo uweze kukamilika hadi kufikia mwaka 2025 ili uanze kutoa huduma kwa wananchi.

Sauti ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa eneo la Kazegunga wameomba serikali kupitia Wizara ya Maji kuongeza kasi ya usambazaji wa maji kwa wananchi.

Sauti za baadhi ya wananchi wa eneo la kazeg