Joy FM

Tani 3.6 za bidhaa bandia zateketezwa na TBS Kigoma

25 June 2024, 09:55

Baadhi ya bidhaa zisizokuwa na ubora ambazo zimekamatwa na kuteketezwa na TBS kanda ya magharibi kigoma

Jamii mkoani Kigoma imetakiwa kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara kubaini na kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na uingizaji wa bidhaa zisizokuwa na ubora kwa mamlaka husika ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Na Emmanuel Matinde -Kigoma

Bidhaa mbalimbali zenye uzito wa tani 3.6 zikiwa na thamani ya shilingi milioni 34 zikiwemo vyakula, vipodozi vyenye viambata vya sumu, nguo za ndani za mitumba na vilainishi vya magari zimeteketezwa mkoani Kigoma na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutokana na kutokidhi viwango vya ubora.

Ni baadhi ya bidhaa feki zikiwa zinamwagwa na gari tayari kwa kuchomwa na TBS, Picha na Emmanuel Matinde

Afisa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS Kanda ya Magharibi Elisha Meshack, amesema bidhaa hizo zimenaswa katika maduka takribani mia moja kote mkoani Kigoma, kufuatia operesheni na kaguzi za kawaida zilizofanywa na TBS kwa kushirikiana na idara zingine za serikali.

Sauti ya Afisa Udhibiti Ubora TBS Kanda ya Magharibi.

Afisa Udhibiti Ubora TBS Kanda ya Magharibi Peter Musiba amesema wataendelea kutumia njia na mbinu mbalimbali kukabiliana na wauzaji wa bidhaa zisizokidhi viwango na zile zilizopigwa marufuku kutumika nchini huku afisa afya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Roza Aloyce Choma, akitahadharisha juu ya madhara ya kutumia bidhaa hizo.

Sauti ya Afisa Udhibiti Ubora TBS Kanda ya Magharibi Peter Musiba, na afisa afya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Roza Aloyce Choma
Ni moto ukiteketeza bidhaa feki zilizokamatwa na TBS kanda ya magharibi

Baadhi ya wananchi walioshuhudia uteketezaji wa bidhaa hizo uliofanyika katika eneo la Businde Manispaa ya Kigoma Ujiji, walikuwa na haya ya kusema.

Sauti ya wananchi walioshudia uchomaji wa bidhaa feki