Mpanda FM

TRA Katavi wafanya usafi pamoja na kutoa msaada Kwa wagonjwa

26 November 2022, 6:17 am

MPANDA
Katika kuadhimisha wiki ya Mlipa kodi Mamlaka ya ukusanyaji mapato [TRA] mkoani Katavi wametembelea hospitali mpya ya mkoa na kufanya usafi pamoja na kutoa msaada kwa wagonjwa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Meneja wa mamlaka ya ukusanyaji mapato mkoa wa katavi, Jackob Timoth Mtema ngombe amesema lengo la kufanya hivyo ni kurudisha shukrani kwa walipa kodi na kuitambua michango yao katika ukusanyaji mapato.

Akizungumza baada ya zoezi la usafi na kukabidhi zawadi kukamilika Mwajuma mbaga muuguzi mfawidhi hospitali ya rufaa Katavi ameshukuru kwa zoezi la usafi kwani limesaidia kutengeneza mazingira safi kwa hospitali mpya na kuongeza faraja kwa wagonjwa.

Wiki ya mlipa kodi mkoani Katavi imeadhimishwa kwa kufanya usafi hospital mpya, kuwatembelea wagonjwa na inatarajiwa kufikia kilele November 25 kwa kufanyika kwa bonanza la michezo kwenye viwanja vya azimio mkoani hapa.