Wakristo watakiwa kuendelea kuwasaidia watu wenye uhitaji
17 December 2024, 12:43
Jamii na wadau mbalimbali wametakiwa
Kanisa la FPCT Murusi Galilaya lililopo Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma limetoa msaada kwa watu wenye uhitaji ikiwemo chakula, nguo, Sabuni na Viatu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tatu.
Msaada huo umetolewa katika ibada maalum ya kuwaombea na kuwasaidia Wahitaji hao kanisani hapo.
Ambapo Katibu wa kanisa la FPCT Murusi Thomas Masama amesema ni vizuri kumsaidia muhitaji kwa kidogo ulicho nacho ndiyo maana wao kama kanisa wamekuwa na desturi ya kila mwaka kuwasidia kwa vitu mbali mbali wanavyokuwa navyo.
Sauti ya Katibu wa kanisa la FPCT Murusi
Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Jafet Gileadi amesema wamefanya huduma hiyo kwa kuwasaidia na kuwatia moyo watu wanaoishi katika mazingira magumu maana neno la Mungu linawaagiza kufanya hivyo.
Sauti ya Mchungaji Kiongozi FPCT Murusi
Diwani wa kata ya Murusi Fanuel Kisabo amesema kwa kidogo walichokipata wahitaji hao kiwe chachu ya kufanya matendo mema kwa wengine yatakayoweza kuwafikisha mbinguni pia amewaomba kumshirikisha katika zoezi la mwaka ujao watakapoanza kuchangia ili aweze kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Sauti ya Diwani Kata ya Murusi
Nao baadhi ya watu wenye uhitaji waliopewa msaada huo wameshukuru kwa msaada waliyopewa maana imekuwa faraja katika maisha yao.
Sauti za Watu waliopata msaada
Hii ni mara ya pili kwa kanisa hilo kufanya tukio hilo maana mwaka jana waliwasaidia watu wenye uhitaji zaidi ya 300 na mwaka huu wamewasaidia watu wenye uhitaji 185.