Joy FM

JKT Mtabila yaleta faraja wilayani Kasulu

10 December 2024, 15:18

Jeshi la Kujenga Taifa JKT Mtabila wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameshiriki zoezi la kuchangia damu kwa hiari katika hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Kasulu Nyamnyusi ili kuwasaidia wahitaji wa damu wanaofika katika hospitali hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutamatika kwa  zoezi la kuchangia damu kwa hiari pamoja na zoezi la usafi wa mazingira katika hospitali ya halmshauri ya wilaya ya Kasulu Nyamnyusi, Kaimu Mganga Mkuu wa halmshauri hiyo Dokta Mageni Pondamali amesema bado kuna uhitaji  mkubwa wa damu hivyo ni muhimu jamii na Watanzania kuendelea kujitokeza kuchagia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wahitaji.

kaimu mganga mkuu wa halmshauri Dokta Mageni Pondamali

Kwa upande wake mratibu wa huduma za maabara halmashauri wa wilaya ya Kasulu Dkta Jasmini Meru ameeleza kiasi cha Damu kilichopatikana na kueleza namna itakavyosaidia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua pamoja ,wahanga wa ajari pamoja na wagonjwa wa Siko seli wanaofika kwa ajili ya matibabu katika hospitali hiyo.

Mratibu wa huduma za maabara Dkta Jasmini Meru

Mkuu wa kitendo cha udhibiti wa taka na usafi wa mazingira  halmshauri ya vilaya ya kasulu bw. Ndelekwa Vanica akizungumza kwa niaba  ya mkurugenzi wa halmshauri hiyo Amepongeza wananchi pamoja JKT Mtabila kwa kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu pamoja na zoezi la usafi wa mazingira na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana katika shughuli mbalimbali.

Bw. Ndelekwa Vanica

..