Joy FM

DC Kigoma aagiza watumishi 4 kusimamishwa kazi

7 October 2024, 12:55

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua akisikiliza maelezo wakati alipotembelea hospitali ya wilaya manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Ofisi ya Mawasiliano Manispaa ya Kigoma Ujiji

Watumishi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kufanya kazi kwa weledi pasipo kuingiza hasara kwa serikali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Na Joesphine Kiravu

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Mohamed Chuachua ameonesha kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya wilaya ya Manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na mchakato uliotumika kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzai wa jengo la utawala na kumwagiza mkurugenzi wa manispaa kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi Afisa Utumishi, Afisa Tehama, Afisa mMnunuzi kwa kosa la kutaka kuisababishia hasara serikali.

Mkuu wa Wilaya Kigoma akiwa katika ukaguzi wa hospitali ya wilaya ya manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Ofisi ya Mawasiliano Kigoma

Amesema watumishi hao walitumia njia isiyo sahihi kumpata mkandarasi na kuagiza mchakato uanze upya ili kumpata  mkandarasi atakaejenga jengo la utawala.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Mohamed Chuachua

Awali akiwa katika ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Kigoma ujiji Dkt. Chuachua ametilia shaka utekelezaji wa mradi huo na kuiagaiza Taasis ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kufanya uchunguzi kwenye mradi huo kwa kupitia nyaraka zote tangu kuanza mradi huo.

Sauti na Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Mohamed Chuachua

Akisoma taarifa kuhusu mradi huo Kaimu mganga mkuu Manispaa ya Kigoma ujiji Omary Kibwana amesema mpaka sasa wamepokea kiasi cha shilingi billion 1.3 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Sauti ya Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Kigoma Ujiji Omary Kibwana

Mkuu wa wilaya amehitimisha ziara yake kwa kuzungumza na watumishi wa manispaa ya Kigoma ujiji nakuwataka kufanya kazi kwa weledi pasipo kuingiza hasara kwa serikali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi